Quantcast
Channel: AutomobileHeat » css
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Yanga awa Mbabe kwa Mtibwa Sugar Ingawa wote ni wababe.

$
0
0

Mchezo wa mwisho wa Kundi B katika michuano ya Kombe la Mapinduzi umepigwa usiku huu katika dimba la  Amaan  visiwani  Zanzibar , huu ni mchezo ambao umezikutanisha timu za  Mtibwa Sugar  dhidi ya  Dar Es Salaam   Young African , licha ya kuwa  Mtibwa  na Yanga  wamefuzu hatua ya nusu fainali, haukuwa mchezo rahisi kwa timu zote mbili. Kila timu ilionekana kusaka ushindi ili ipate nafasi ya kuongoza Kundi B nusu fainali ikutane na timu dhaifu ya Kundi A, yaani mshindi wa pili.  Mtibwa  walianza kwa kasi na dakika ya 10  Shiza Kichuya  akafanikiwa kupachika goli nyavuni kwa shuti kali la nje ya 18,  Yanga  ambao walikuwa na kikosi makini. Hawakuwa na papara licha ya kuwa walikuwa nyuma kwa goli moja kwa bila, hadi pale dakika ya 42 mshambuliaji wao wa kimataifa wa  Niger   Issofou Boubacar  kupachika goli la kwanza.  Yanga  walizidi kuonesha dhamira ya kuhitaji ushindi katika mechi hii, licha ya kuwa tayari walikuwa wamefanikiwa kutinga nusu fainali. Kocha wa  Yanga   Hans van Pluijm  alifanya mabadiliko yaliozaa matunda kwa kumtoa Amissi Tambwe  na kumuingiza  Malimi Busungu  aliyeenda kupachika goli la pili, na kuufanya mchezo umalizike kwa  Yanga  kuibuka wa goli 2-1. Kwa matokeo hayo  Yanga anasubiri mshindi wa pili wa Kundi A kucheza nae hatua ya nusu fainali, wakati  Mtibwa Sugar  wakimsubiri mshindi wa kwanza wa Kundi A.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Trending Articles