Quantcast
Channel: AutomobileHeat » css
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Mbunge Deo Filikunjombe na baba yake Jerry Silaa wamefariki kwa ajali ya Helikopta.. #RIP

$
0
0

Kumekuwa na mvutano wa taarifa zinazoripotiwa kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya  October 15 2015  katika Msitu wa Mbuga ya Selous, pembeni ya Mto Ruaha. Jerry Silaa  amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge  Deo Filikunjombe pamoja na baba yake, Mzee  William Silaa  ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo > > >  “ Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani “ —  jerrysilaa Hii ni picha ya zamani,  Zitto Kabwe  akiwa na Marehemu  Deo Filikunjombe . “ Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr. Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS ” > > >   jerrysilaa Marehemu  Deo Filikunjombe  na baadhi ya Wapigakura wake wa Jimbo la Ludewa, Mkoa wa Njombe. Reporter wa millardayo.com amemtafuta  Jerry Silaa   lakini simu yake ilipokelewa na Msaidizi wake,  Fadhili Idd  ambaye amesema ni kweli wanethibitishiwa kuhusu taarifa ya Msiba na wanajiandaa na taratibu nyingine kwa sasa. RIP Marehemu  Captein William Silaa  & Mbunge  Deo Haule Filikunjombe

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Trending Articles