Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Maamuzi mengine leo kutoka kwa Waziri wa Magufuli

Image may be NSFW.
Clik here to view.

March 23 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ime kutana na Baraza la Wazee wa Dar es salaam na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika jamii. Katika kutatua changamoto zinazowakabili wazee, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeonyesha imedhamiria kutoa kipaumbele kwa wazee na imesisitiza kusimamia Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure kwa wazee. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu amezungumza na waandishi wa habari na kusema…. > > ’ ku husu huduma kwa wazee hasa matibabu tunataka kuwathibishia bado inabaki kuwa ni sera ya Serikali  na kwamba wazee Tanzania wanatakiwa  kupata matibabu bure, kuanzia gharama ya kumuona Daktari, vipimo na Dawa. Naendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure ikiwemo kuanzisha dirisha la wazee ‘. > > > ’ na kuonyesha kwamba nimedhamiria nimeshaongea na watu wa bima ya afya mwezi ujao tutatoa matangazo ambayo tutaweka katika vituo vyote vya Serikali ‘Mzee kwanza, Mzee alikuwa kama wewe na wewe utakuwa kama yeye, tafadhali toa kipaumbele cha huduma kwa wazee’ tayari tumeshaaanza tunatafuta siku ya kuyazindua ili kuendelea kuhamasisha kipaumbele kwa wazee ‘

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Trending Articles