Quantcast
Channel: AutomobileHeat » css
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Baada Adam Johnson kukiri kujihusisha na mapenzi na binti U-16, klabu na Adidas imeamua hivi, kabla ya hukumu

$
0
0

February 11 stori zilizoingia kwenye headlines katika soka la  Uingereza  ambalo linaaminika kuwa na mashabiki wengi wanaopenda Ligi hiyo, ni kuhusu winga wa zamani wa klabu ya  Man City  anayeichezea klabu ya  Sunderland  kwa sasa  Adam Johnson kuvunjiwa mkataba wake na klabu hiyo na wadhamini wake  Adidas . Klabu ya  Sunderland  imefikia maamuzi hayo baada ya winga huyo kukiri kuhusika kumrubuni kimapenzi msichana mwenye umri chini ya miaka 16, kitu ambacho ni kinyume cha sheria, winga huyo mwenye umri wa miaka 28 alikiri kosa la kumrubuni kwa njia ya mtandao (grooming) binti huyo ambae ni mwanafunzi, kukutana nae kumshika maungo yake na kumbusu. Kosa hilo limefanya klabu yake ya  Sunderland  kuvunja mkataba nae lakini pia wadhamini wake  Adidas  wamevunja mkataba nae, kwa kukiri kosa hilo  Adam Johnson  huenda akahukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela na kama akikiri makosa yote huenda akafungwa miaka 14 jela.  Adam   Johnson  ambaye kesi hiyo ilianza toka mwaka jana alijiunga na klabu ya  Sunderland  mwaka 2012 kwa dau la pound milioni 10 akitokea klabu ya  Man City . Kesi hiyo itaendelea tena Ijumaa ya February 12.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1303

Trending Articles